Uturuki yatoa pole kwa Afghanistan

Uturuki yatuma ujumbe wa rambirambi kwa watu waliopoteza maisha kwenye shambulizi la bomu Afghanistan

1632073
Uturuki yatoa pole kwa Afghanistan

Uturuki imetuma ujumbe wa pole na rambirambi kwa wale waliopoteza maisha katika shambulizi la bomu la kigaidi lililotokea nchini Afghanistan wakati wa futari.

Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje, iliandikwa kwamba Uturuki imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kufariki kwa watu wengi ikiwa ni pamoja na wanafunzi wa shule za upili, waliopoteza maisha na kujeruhiwa katika shambulizi la bomu huko Pul-i Alem, wilaya ya kati ya mkoa wa Logar wa Afghanistan, wakati wa iftar.

Katika taarifa hiyo, pia iliandikwa,

"Tunalaani na kukemea wahusika wa shambulizi hili la kigaidi na tunatumahi kuwa watawajibika mbele ya haki. Tunawaombea Mungu awarehemu wale wote waliopoteza maisha katika shambulizi hilo, na kuwatakia afueni ya haraka wale waliojeruhiwa. Tunatoa pole zetu kwa rafiki zetu na ndugu zetu wananchi wa Afghanistan na Serikali kwa ujumla."

Katika shambulizi hilo lililotekelezwa kwa kutumia gari lililosheheni mabomu na kulipuliwa hapo jana wakati wa futari kwenye jimbo la Logar nchini Afghanistan, watu 30 walipoteza maisha na zaidi ya 90 walijeruhiwa.Habari Zinazohusiana