Uwanja wa ndege wa Istanbul waongoza barani Ulaya

Kulingana na ripoti ya Eurocontrol ya miezi minne ya kwanza ya 2021

1631476
Uwanja wa ndege wa Istanbul waongoza barani Ulaya

Kulingana na ripoti ya Eurocontrol ya miezi minne ya kwanza ya 2021 (Januari-Aprili), safari za ndege 63,064 zilifanywa katika Uwanja wa ndege wa Istanbul.

Idadi hii ya safari imeufanya uwanja wa ndege wa Istanbul kuwa uwanja wa kwanza kwa kuwa na safari nyingi za ndege barani Ulaya katika miezi minne ya kati ya Januari na Aprili 2021.

Baada ya uwanja wa Istanbul, unafuata uwanja wa ndege wa Paris Charles de Gaulle na safari za ndege 53 921.

Amsterdam Schiphol imechukua nafasi ya tatu na ndege 52,532, Frankfurt na ndege elfu 52 464, na viwanja vya ndege vya Madrid Barajas vilivyo na ndege 42,543.

Katika taarifa iliyotolewa kwenye akaunti ya media ya kijamii ya IGA, kiongozi wa Uwanja wa ndege wa Istanbul, alisema kuwa: "Sisi ndio kiongozi huko Ulaya katika miezi 4 ya kwanza ya 202.Ni fahari yetu sote. "Habari Zinazohusiana