Tatar kukutana na Erdoğan mwezi huu

Rais wa KKTC Ersin Tatar atangaza mpango wa kukutana na Rais Erdoğan Aprili 26

1626225
Tatar kukutana na Erdoğan mwezi huu

Rais wa Jamhuri ya Kİturuki ya Cyprus ya Kaskazini (KKTC) Ersin Tatar, alitangaza kuwa watakutana na Rais Recep Tayyip Erdoğan huko Ankara tarehe 26 Aprili.

Tatar alitoa taarifa hiyo wakati wa mkutano wa Baraza la Mawaziri, ambao aliongoza kwa mara ya kwanza baada ya kuchukua madaraka.

Tatar alitangaza kwamba atakutana na Rais Erdoğan tarehe 26 Aprili siku ya Jumatatu, kabla ya mkutano wa wa 5+UN kufanyika kuanzia 27 hadi 29 Aprili chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa (UN) na mamlaka ya dhamana ya Uturuki, Ugiriki na Uingereza.

Tatar alisema, "Sera mpya itafunuliwa huko Geneva, Uswisi pamoja na Uturuki, upande wa Cyprus ya Kituruki, kulingana na usawa wa serikali mbili za nchi hizi, kwa kuwa hii ndio njia pekee na sahihi katika kutafuta suluhisho."Habari Zinazohusiana