Uturuki yatuma ujumbe wa rambirambi kwa Chad

Serikali ya Uturuki yatuma ujumbe wa rambirambi kwa Chad kufuatia kifo cha Rais Idris Debi Itno

1625346
Uturuki yatuma ujumbe wa rambirambi kwa Chad

Uturuki imetuma ujumbe wa rambirambi kufuatia kifo cha Rais wa Chad Idris Debi kilichotokea kama matokeo ya mapigano ya kijeshi na vikundi vya upinzani nchini humo.

Katika taarifa iliyoandikwa na kutolewa na Wizara ya Mambo ya Nje, ilitangazwa,

"Tunatuma salamu za rambirambi kutokana na kifo cha Idris Debi Itno ambaye alichangia urafiki na uhusiano wa kindugu kati ya Uturuki na Chad, na tunatoa pole zetu za dhati kwa serikali."

Katika taarifa hiyo, ilielezwa kwa masikitiko kuwa Itno alipoteza maisha kutokana na mapigano dhidi ya wapinzani wenye silaha.

Msemaji wa Jeshi la Chad Azem Bermandoa Agouna, alitangaza katika televisheni ya kitaifa mnamo Aprili 20 kwamba Itno, mwenye umri wa miaka 68, alishiriki katika operesheni dhidi ya waasi wa Chad Change and Unity Front kaskazini mwa nchi hiyo mwishoni mwa wiki ambapo baadaye alifariki baada ya kujeruhiwa katika mapigano hayo.Habari Zinazohusiana