Balozi wa Uturuki akutana na jamii ya Waislamu Marekani

Balozi wa Uturuki Hasan Murat Mercan akutana na wawakilishi wa jamii ya Waislamu New Jersey nchini Marekani

1618522
Balozi wa Uturuki akutana na jamii ya Waislamu Marekani

Balozi wa Uturuki mjini Washington Hasan Murat Mercan, alikutana na wawakilishi wa jamii ya Waislamu katika jimbo la New Jersey nchini Marekani.

Akizungumza kwenye mkutano uliofanyika katika jiji la Paterson, Mercan alielezea kufurahishwa kwake na ushirikiano wa karibu wa kikazi wa jamii ya Kituruki nchini Marekani na jamii ya Waislamu.

Mkutano huo ulioandaliwa na Kamati ya Uendeshaji ya Kituruki nchini Marekani (TASC), ulihudhuriwa na Balozi Msaidizi wa New York Reyhan Özgür, Mshauri wa Huduma za Dini Bilal Kuşpınar, Mwenyekiti mwenza wa jamii ya TASC Halil Mutlu na maafisa wengine wakuu, pamoja na wawakilishi wa mashirika ya jamii ya Waislamu huko New York na New Jersey.

Akizungumzia shida za kawaida zinazokabiliwa na jamii ya Marekani, Mercan alisisitiza kwamba wanapaswa kuchukua hatua pamoja kuzitatua shida hizo. Aliongezea kusema "Lazima tuwaonyeshe watu wa Marekani uzuri wetu jinsi ulivyo,na  kwamba hatutaki chochote isipokuwa uzuri wa nchi hii na sisi ni sehemu muhimu katika jamii hii."

Baada ya mkutano wake na viongozi wa jamii ya Waislamu, Balozi Mercan alitembelea sehemu za kazi za raia wa Kituruki wanaoishi New Jersey na kupokea taarifa juu ya kazi zao.Habari Zinazohusiana