Msaada wa vifaa vya kijeshi kwa Albania

Uturuki yatoa msaada wa vifaa vya kijeshi kwa Albania

1544351
Msaada wa vifaa vya kijeshi kwa Albania

Uturuki imetoa msaada wa vifaa vya bunduki na sare za magwanda kwa jeshi la kitaifa la Albania. 

Uturuki imetoa msaada huo wa vifaa vya kijeshi kwa Albania kufuatia mkataba uliosaniwa kati ya nchi hizo mbili. 

Wizara ya Ulinzi wa Taifa ilitoa maelezo na kusema,

"Katika mkataba wa misaada uliotiwa saini kati ya Uturuki na Albania, vifaa vya bunduki vilivyoundwa ndani ya nchi na kufanyiwa majaribio 42 na NATO kwa mafanikio, pamoja na sare za magwanda ya kijeshi kwa ajili ya kikosi cha majini cha Albania, vimewasilishwa kwa viongozi mjini Tirana." Habari Zinazohusiana