Mturuki aliyeshambuliwa Yemen aletwa Uturuki

Mhudumu wa shirika la Türk Kızılay aliyejeruhiwa Yemen aletwa Uturuki

1515415
Mturuki aliyeshambuliwa Yemen aletwa Uturuki

Mhudumu mmoja wa shirika la Türk Kızılay Ali Can Budak aliyejeruhiwa kwa silaha nchini Yemen, ameletwa Ankara kwa ndege maalum ya kusafirishia wagonjwa inayomilikiwa na Wizara ya Afya.

Ali Can Budak mwenye umri wa miaka 29 aliyekuwa akihudumu kwenye timu ya misaada ya Türk Kızılay nchini Yemen, alishambuliwa na watu wasiojulikana katika mji wa Aden na kujeruhiwa vibaya.

Baada ya mashambulizi hayo, Budak alifikishwa kwenye hospitali ya Al Naqib mjini Aden na kufanyiwa upasuaji wa ubongo, ambapo baadaye Wizara ya Afya ya Uturuki ikachukuwa uamuzi wa kutaka kumsafirisha nchini ili kuendeleza matibabu.

Baada ya maandalizi kukamilika, Wizara ya Afya ilituma ndege ya kusafirishia wagonjwa mjini Aden nyakati za asubuhi ili kumchukuwa Budak.

Hatimaye Budak akasafirishwa hadi kwenye uwanja wa ndege wa Ankara Esenboğa kutoka Aden, na kisha akapelekwa kwenye hospitali ya Taalum na Utafiti ya Ankara ili kuendeleza matibabu.

Hali ya afya ya Budak imetangazwa kuendelea vyema.Habari Zinazohusiana