Gari la kwanza la kuruka angani "Cezeri" la Uturuki lafanya majaribio kwa mafaanikio

Gari la kwanza la kuruka angani "Cezeri" la Uturuki lafanya majaribio yake ya kwanza kwa mafaanikio

1491629
Gari la kwanza la kuruka angani "Cezeri" la Uturuki lafanya majaribio kwa mafaanikio

Gari la kwanza la kuruka angani "Cezeri" la Uturuki lufanya majaribio kwa mafaanikio katika hatua zake za kwanza.

Katika majaribio yake ya kwanza  ya  gari au kipandwa cha angani ambacho kimetengenezwa na shirika la Baykan kwa jina la "Cezeri" kimeonesha matumaini kwa  kufaulu majaribio yake ya kwanza.

Taarifa zilizotolewa na  shirika ambalo linahusika na utafiti wa vifaa vya teknolojia zimesema kuwa   majaribio ya gari hilo  yalianza kufanyika Ijumaa wiki iliopita Septemba  11 na kuonesha matokea yaliokuwa  yakitarajiwa.

Cezeri imetengenezwa na mafundi wa kituruki na kurushwa  kwa mita  10 wakati wa majaribio ya tuleo lake la kwanza la utafiti la uzito wa kilomita 230.

Mkurugenzi  katika kitengo cha ufundi Baykar, Selçuk Bayraktar amenukuliwa akisema kwamba  " tutaendelea kuunda vifaa hivyo katika  nyakati zijazo  baada ya kuonekana kwa ufanisi huo na  vifaa ambavyo binadamu atakuwa na uwezo  wa kuwemo kwa muda katika vipandwa hivyo.

Gari au kipandwa hicho kitakuwa na umuhimu mkubwa  kwa mabadiliko  makubwa katika uchukuzi mijini kwa raia.

Gari hilo  ambalo linatumia umeme  lina mfumo wa roboti ya kisasa ambayo itaongezewa mfumo mwingine.

Cezeri ina uwezo wa kusafiri mwendo wa kilomita 100 kwa muda wa saa moja katika umbali wa mile 2000 na uwezo wa kujitegemea kilomita 70 hadi 80  kwa saa moja likiwa angani.Habari Zinazohusiana