Uturuki yakemea shambulizi la kigaidi nchini Mali

Uturuki kupitia wizara yake ya mambo ya nje imelaani vikali shambulizi la kigaidi lilitekelezwa nchini Mali

1382458
Uturuki yakemea shambulizi la kigaidi nchini Mali

 
Uturuki kupitia wizara yake ya mambo ya nje imelaani vikali shambulizi la kigaidi lilitekelezwa nchini Mali.

Askari 29 wa Mali wameuawa katika shambulizi la kigaidi lililowalenga Kaskazini mwa Mali.

Uturuki imelaani shambulizi hilo lililopelekea kuuawa kwa wanajehsi 29 wa Mali waliokuwa katika kambi yao Kaskazini mwa Gao.

Katika shambulizi  hilo wanajeshi wengine watano wameripotiwa kujeruhiwa.

Habari iliochapishwa na ofisi ya waziiri wa mambo ya nje wa Uturuki imefahamisha kusikitishwa na  maafa yaliosababishwa na shambulizi hilo  dhidi ya kambi ya  jeshi Gao nchini Mali.

Salamu za rambi rambi zimetolewa  kwa familia za wanajeshi waliopoteza maşsha katika shambulizi hilo.
 Habari Zinazohusiana