Je wajua supu ya kwanza kutengenezwa ulimwenguni?

Supu ya "Tarhana"

Je wajua supu ya kwanza kutengenezwa ulimwenguni?

Je! Wajua kuwa "tarhana” iliyotengenezwa na Waturuki wa Asia ya Kati ni moja ya supu za kwanza kutengenezwa duniani?

Tarhana ni bidhaa inayopatikana kwa kuchanganya, kukausha, na kusaga unga, yoghurt, mboga na viungo. Supu ya tarhana iliyotengenezwa na Waturuki wa Asia ya Kati ni moja ya supu za kwanza zilizotengenezwa ulimwenguni. Hakuna taarifa kamili juu ya jina la tarhana kuletwa Mashariki ya Kati na Anatolia. Wagiriki huita Tarhana kwa jina la "trhana”.

Kuna uvumi juu ya asili ya neno Tarhana: Simulizi inayokubalika zaidi ni kwamba inatokana na neno “dar hane” ikimaanisha nyembamba ... ... Katika mwezi wa Ramadhani, Sultani alikua akitembelea maeneo maskini. Akawa mgeni katika nyumba moja aliyopita wakati wa iftar.Alipewa supu na mkate.

Sultan aliipenda sana supu hiyo na kuuliza ni supu ya nini.

Bibi kizee huyo aliyekuwa ndiye mwenye nyumba alijibu kuwa supu ile ni ya tarhana na kumtaka Sultan afurahie chakula chake.

" Kulingana na hadithi, supu hii, inayoitwa “dar hane”, imegeuka kuwa tarhan jinsi wakati ulivyoenda.

Tarhana tofauti tofauti hutengenezwa sana katika mji unaoitwa Kahramanmaş nchini Uturuki.

Tarhana pia ni mashuhuri katika maeneo kama

Uşak, Afyonkarahisar, Malatya na Bandırma, Gönen, Gediz, wilaya za Beypazarı pia ni maarufu kwa tarhana yao.Habari Zinazohusiana