Umuhimu wa kwenda jeshini nchini Uturuki

Hafla ya kwenda jeshini

1305709
Umuhimu wa kwenda jeshini nchini Uturuki

Je! Wajua kuwa kuna utamaduni wa Kituruki wa kusherehekea pale mabadiliko fulani katika maisha yanapotokea na hasa sherehe ya kwenda  jeshini ina umuhimu wa kipekee nchini humo?

Katika jamii yetu, huduma ya kijeshi, ambayo ina tamaduni iliyoanzishwa kwa muda mrefu, inachukuliwa kama jukumu takatifu. Kuwa mwanajeshi kunahusishwa na kuwa mtu mwenye heshima na wema. Hasa vijijini wale ambao hawafanyi wadhfa wao wa kijeshi hawakaribishwi na wala maneno yao hayazingatiwi.

Sherehe maalumu hufanyika mwanzoni na mwisho wa jeshi na hupewa umuhimu mkubwa katika jamii.

Sherehe za kumuaga mtu anapoenda jeshini na kumkaribisha napotoka jeshini hutofautiana kikanda.

Mojawapo ya mazoea ya kawaida katika kila mkoa wa nchi hiyo ni mwaliko wa vijana wanaorudi kutoka jeshi kwa chakula cha jioni wakijumuika na ndugu zao pamoja na marafiki. Chakula hiki huandaliwa sio tu kwa ajili ya kijana aliyetokea jeshi , lakini pia kwa familia yake. Ni kawaida pia kufurahiya wakati wa kula na baada ya kula.Habari Zinazohusiana