Je wajua?

Mchezo wa kivuli wa Karagöz

Je wajua?

Karagöz ni mchezo wa kivuli kulingana na harakati za maumbo ya watu, wanyama au bidhaa zilizotengenezwa kwa ngozi ya ngamia au nyati kwenye skrini nyeupe kwa msaada  wa mwanga. Jina la mchezo, huitwa kichwa cha Karagöz (Jicho jeusi).

Asili ya mchezo huu wa kivuli inasemekana kuanzia nchi za Kusini Mashariki mwa Asia.

Kuna utata wa kujua ni vipi mchezo huu ulitoka Kusini Mashariki mwa Asia mpaka kufika nchini Uturuki.Kuna uwezekano wa kuwa mchezo huu uliletwa na wahamiaji.

Kuna wanaoamini ya kuwa mchezo huu wa kivuli uliletwa na Sultan Yavuz Selim wa Misri katika mwaka wa 1517 baada ya kuruhusu wasanii kuingia nchini.

 

 Habari Zinazohusiana