Muanzilishi wa Amazon avunja rekodi kwa kununua kasri la gharama zaidi kupata kutokea

Jack Bezos anunua kasri la mmoja wa waanzilishi wa studio za kurekodia filamu za Warner bros lililopo mtaa wa Beverly Hills jijini Los Angeles

Muanzilishi wa Amazon avunja rekodi kwa kununua kasri la gharama zaidi kupata kutokea

Muanzilishi wa shirika la Amazon, linalojihusisha na biashara ya mtandaoni, Jeff Bezos amevunja rekodi ya manunuzi kwa kununua kasri la thamani ya dola milioni 165 lililopo mtaa wa Beverly Hills, Los Angeles nchini Marekani.

Kwa mujibu wa habari iliyochapishwa na jarida la Forbes, Kiasi cha dola milioni 165 alichokilpa Bezos kununua jumba lililojengwa mwaka 1937 na mmoja wa waanzilishi wa studio za filamu za Warner Bros, Jack Warner, ndio kiasi kikubwa zaidi kulipwa kwa ajili ya manunuzi ya kasri kilichopata kufanywa jijini Los Angeles.

Kasri hilo lipo kwenye ardhi ya ukubwa wa mita za mraba elfu 36, limejengwa katika mtindo wa ujenzi wa Georgia, ndani ya eneo hilo kuna makasri mawili kwa ajili ya wageni, shamba la mbegu 1, majumba ya mboga mboga 3,  kiwanja cha tenis, bwawa la kuogelea, uwanja wa golfu, na gereji ya magari yenye kituo chake cha kujazia mafuta.Habari Zinazohusiana