Qatar kuwekeza mamilioni ya dola Ujerumani

Qatar imetoa uamuzi wa kuwekeza mabilioni ya dola nchini Ujerumani.

Qatar kuwekeza mamilioni ya dola Ujerumani

Qatar imetoa uamuzi wa kuwekeza mabilioni ya dola nchini Ujerumani.

Hayo yamezungumzwa na waziri wa fedha wa Qatar katika gazeti la uchumi la "Handelsblatt" la Ujeruamani siku chache kabla ya ziara ya Emir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani mjini Berlin.

Waziri wa fedha wa Qatar amesema kuwa nchi yake ina imani na Ujerumani katika suala zima la uchumi na kwamba inaliamini soko lake.

Isitoshe,Berlin ilisimama sambamba na Doha wakati wa mgogoro wa mataifa ya Ghuba.

Qatar imewekeza zaidi ya euro bilioni 20 katika makampuni ya Ujerumani kama Volkswagen, Deutsche Bank, Siemens, Hochtief na SolarWorld ndani ya miaka 30 iliyopita.

Kufanyika kwa kombe la dunia 2022 nchini Qatar kumetoa fursa pia kwa makampuni mengi ya Ujerumani kusimamia miradi ya kutengeneza miundombinu nchini humo.

Mwezi uliopita Qatar ilitangaza kuwekeza $ 15 billioni nchini Uturuki.

 Habari Zinazohusiana