Msemaji wa serikali ya Uturuki azungumzia hali ya uchumi

Ibrahim Kalın azungumzia hali ya uchumi  na kusema kuwa Uturuki  haipo katika vita vya kiuchumi

Msemaji wa serikali ya Uturuki azungumzia hali ya uchumi

 

Msemaji wa ikulu mjini Ankara Ibrahim Kalın asema kuwa Uturuki haipo katika vita vya kiuchumi ila haitofumbia macho mashambulizi dhidi yake.

 Katika mkutano na waandishi wa habari, Ibrahim Kalın  amezungumza kuhusu uchumi wa Uturuki  kwa kusema kuwa  sekta  hiyo haijatetereka  na kwa sasa ipo katika  hali ya kuridhisha.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari , Kalın amezungumzia pia  uamuzi wa  kususia bidhaa kutoka nchini Marekani.  Ibrahim Kalın ameendelea akifahamisha kuwa Uturuki haipo katika vita vya kuichumi   na kusema kuwa haitofumbia macho  mashambulizi yanayolenga sekta yake ya uchumi. 

Kalın amesema kuwa anataraji kuwa  mgogo uliotokea katika ya Uturuki na Marekani utatatuliwa hivi karibuni na kuitolea wito Marekani  kuheshimu  vyombo vya sheria vya Uturuki.

Kalın amewaambia waandishi wa habari kwamba utawala wa Trump, utawala wa Obama  haukuweza kutatatua  masuala muhimu ya usalama kwa Uturuki  kufuatia matendo ya kundi la kigaidi la PKK na kundi la wahaini wa FETÖ.

Rais wa Uturuki atazungumza  kwa njia ya simu na kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Msemaji wa ikulu amezungumzia  kuhusu mazungumzo ya amani ya Astana.

 

 Habari Zinazohusiana