Darubini kubwa zaidi duniani yaanza kufanya kazi rasmi

Darubini kubwa zaidi duniani yenye ukubwa sawa na viwanja 30 vya mpira iliyojengwa huko China imeanza kufanya kazi

Darubini kubwa zaidi duniani yaanza kufanya kazi rasmi

Huko nchini China,darubini kubwa zaidi duniani ya mawimbi ya redio iliyopewa jina la FAST ambayo ina ukubwa sawa na viwanja vya mpira 30 imemakamilisha kipindi cha majaribio.

Wanasayansi nchini china wametangaza kwamba darubini hiyo imeanza kutumika rasmi.

Ujenzi wa darubini hiyo kubwa iliyopo katika eneo la Guizhou ulichukua miaka 5 na ulikamilika mwaka 2016.

Gharama za ujenzi wa darubini hiyo ni dola za Marekani milioni 180. Darubini hiyo inatambulika kama jicho la China angani.

Darubini hiyo ina uwezo wa kukusanya taarifa zenye ukubwa wa gigabyte 38 ndani ya sekunde 1. Kwa kutafuta haidrojeni asilia na mawimbi ya radio yanayosambazwa na nyota na kutathimini taarifa hizo itasaidia katika kufanya uchunguzi wa anga.

 


Tagi: FAST , Darubini , China

Habari Zinazohusiana