Mwanasayansi wa vinasaba apotea nchini China

Mwanasayansi aliyedai amefanya mabadiliko kwenye vinasaba na watoto mapacha wamezaliwa baada ya mabadiliko hayo apotea mara baada ya kuwasilisha mada yake hiyo

Mwanasayansi wa vinasaba apotea nchini China

Mwanasayansi wa China  Cienkui Hı, ambaye hivi karibuni alidai kwamba alifanya mabadiliko katika vinasaba  vya embryo amepotea, hajaonekana tena mara tu baada ya mkutano ambao aliwasilisha kazi yake hiyo.

Cienkui Hi, alidai kwamba  watoto wawili mapacha ambao jozi saba za vinasaba vyao walizibadilisha kwa njia za kisayansi walizaliwa mwezi huu.

Kwa mujibu wa gazeti la ABC la Hong Kong linasema baada ya mkutano wa pili wa "International Summit of Human Genome Regulation" ambao Hi aliwasilisha mada hajaonekana tena na hajulikani alipo.

Shirika la afya duniani WHO lilitangaza mnamo Desemba 3, kwamba litaunda jopo maalum kuchunguza madai ya mwanasayansi huyo ambaye alidai amefanya mabadiliko kwenye vinasaba vya vitoto vichanga nchini China.

Taarifa juu ya watoto hao wachanga waliozaliwa baada ya mabadiliko ya vinasaba wamekabidhiwa kwa familia gani au wapo wapi,  zimehifadhiwa kama siri. 


Tagi: China , Cien Hi

Habari Zinazohusiana