Sherehe za siku ya Jamhuri Kapadokya

Watalii wabebwa na maputo ya bendera za Uturuki katika eneo la Kapadokya

1517925
Sherehe za siku ya Jamhuri Kapadokya

Maputo makubwa ya kusafiria angani ya Kapadokya yamepambiwa kwa bendera za Uturuki na kurushwa hewani kwa ajili ya kusherehekea siku ya Jamhuri ya tarehe 29 Oktoba.

Eneo la Kapadokya ambalo ni mojawapo ya vivutio muhimu vya kitalii nchini Uturuki, lilitekeleza usafiri wa maputo makubwa hewani yaliyotundikwa bendera za Uturuki asubuhi ya leo.

Maputo hayo ambayo hutumika kusafirishia watalii wa ndani na nje ya nchi ili kutazama mazingira ya kitamaduni na kiasili kutoka angani, yalipambiwa kwa bendera za Uturuki kwa ajili ya sherehe za maadhimisho ya siku ya Jamhuri ya tarehe 29 Oktoba.

Maandalizi hayo maalum yalifanyika alfajiri ya leo katika mji wa Göreme na baadaye wahudumu wakapamba bendera za Uturuki kwenye maputo hayo kisha yakarushwa hewani kusafirisha watalii kwenye anga ya Kapadokya.

Maputo hayo yalizunguka hewani kuonyesha mandhari ya mabonde, miamba na majabali ya asili yanayovutia kwa muda wa takriban saa moja.Habari Zinazohusiana