Jumba la Asili la Makumbusho mjini Ankara

Je! Unajua kwamba moja ya Jumba kuu la kumbukumbu la Asili lipo Ankara nchini Uturuki?

1516303
Jumba la Asili la Makumbusho mjini Ankara

Je! Unajua kwamba moja ya Jumba kuu la kumbukumbu la Asili lipo Ankara nchini Uturuki?
Haya ni makumbusho ya kwanza na jumba kubwa zaidi la historia ya asili ya Uturuki, yaliyoanzishwa na Kurugenzi ya Utafiti na Uchunguzi wa Madini huko Ankara mnamo 1968.

visukuku vingi vinavyoelezea historia ya asili, miamba, madini na maonyesho ya makumbusho ya madini vinaonyeshwa katika jumba hilo lenye ghorofa tatu.

Ghorofa ya kuingilia ya jumba la kumbukumbu inakaribisha wageni wake na kaulimbiu ya "kusafiri angani". Hapa, kuna fursa ya kujua sayari katika mfumo wa jua kwa karibu na kuchunguza jiwe la mwezi, jiwe la umeme na vimondo.

Visukuku na visukuku vya mimea ya wanyama wenye uti wa mgongo ,dinosaurs zinazokula nyama zilizoanza miaka milioni 140, Tembo wa Maraş na mifupa ya nyangumi wako kwenye ghorofa ya kwanza ya jumba la kumbukumbu.

Walakini Uturuki pia iko kwenye sakafu hii na amabpo inaonyesha wanyama na mimea ya kihistoria .

Katika ghorofa ya pili kuna mawe ya mapambo, sampuli za miamba na mfano wa historia ya madini nchini Uturuki.

Jumba hili la kumbukumbu lina sehemu maalum iliyoundwa kwa wageni wasioona, pia ni la kwanza nchini Uturuki kubeba sifa hiyo.Habari Zinazohusiana