Kanisa la Meryem Ana lasherehekea siku kuu ya Krismas Ankara

Kanisa la Meryem Ana mjini Ankara lasherehekea siku kuu ya Krismas

1329012
Kanisa la Meryem Ana lasherehekea siku kuu ya Krismas Ankara
kilise.JPG
kilisei.JPG
kilis.JPG


Kanisa la Meryem Ana mjini Ankara lasherehekea siku kuu ya Krismas.

Usimamizi wa kanisa Katoliki katika uwakilishi wake mjini Ankara katika Kanisa  ambalo linatambulika kwa jina la Meryem Ana umesherekea siku kuu ya Krismas, siku kuu ambayo huadhimishwa kila ifikapo Disemba 25 kila mwaka.

Siku kuu hiyo husherekewa kuadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo kwa mujibu wa imani ya kikristo.

Viongozi wa kanisa hilo la Meryem Ana Pere Seraphin na Mheshimiwa Charlie wametoa ujumbe wa  umoja na kuomba amani kote ulimwenguni  kwa mungu.

Katika ibada ya misa iliosomwa, wakristo waliohudhuria wamekumbushwa umuhimu wa Krismas na kuomba kujitambua na kuwa mfano katika jamii.
 Habari Zinazohusiana