Rafael Nadal ashinda Roma Open

Rafael Nadal ashinda ubingwa wake wa 10 Roma Open baada ya kumpindua Novak Djokovic

1641047
Rafael Nadal ashinda Roma Open

Mwanatenisi wa Uhispania anayeshikilia nambari 2 ulimwengu Rafael Nadal, alishinda taji lake la 10 katika Mashindano ya  tenisi ya Roma Open kwa kumshinda mwanatenisi nambari 1 ulimwengu kutoka Serbia Novak Djokovic katika fainali ya wanaume.

Mashindano hayo yaliyofanyika kwenye sakafu  za udongo katika uwanja wa michezo wa Foro Italico huko Roma, mji mkuu wa Italia, yalikamilishwa na mechi za mwisho zilizochezwa jana.

Katika fainali ya pekee ya wanaume, wanatenisi mahiri waliotia fora kwenye mashindano haya katika miaka ya hivi karibuni walikutana. Katika mashindano haya, bingwa mara 5 Novak Djokovic na bingwa mara 9 Rafael Nadal walipambana.

Pambano  hilo la mwisho la fainali, ambalo lilichezwa na kusisimua kwa upinzani mkubwa, lilidumu kwa masaa 2 na dakika 49.

Nadal alianza kushinda seti ya kwanza 7-5 licha ya kupata changamoto kubwa. Wakati Nadal hakuweza kuonyesha upinzani katika seti ya 2, Djokovic alishinda seti hiyo 6-1 na matokeo yakawa 1-1 katika mechi hiyo.

Katika seti ya mwisho ya mechi, Nadal alimshinda Djokovic 6-3, na kumaliza mechi hiyo kwa ushindi wa seti 2-1.

Hivyo basi, Nadal alifikia taji lake la 10 katika fainali ya 13 alizocheza kwenye mashindano ya Roma Open.Habari Zinazohusiana