Federer kukosa Miami Open kutokana na jeraha

Roger Federer hatashiriki mashindano ya tenisi ya Miami Open mwaka huu kutokana na jeraha

1593626
Federer kukosa Miami Open kutokana na jeraha

Mswisi Roger Federer, ambaye anajiandaa kurudi kwenye tenisi baada ya kupumzika kwa muda mrefu kutokana na jeraha lake, hatashiriki Mashindano ya Tenisi ya Miami Open mwaka huu.

Katika taarifa iliyotolewa na shirika hilo, ilitangazwa kuwa bingwa wa mwisho mwenye umri wa miaka 39 Federer hatashiriki mashindano ya mwaka huu ambayo yatafanyika Machi 22-Aprili 4, kupitia ujumbe ulioandikwa "Roger, atakosekana mwaka huu. Tukutane mwaka 2022."

Federer ambaye hakuweza kucheza kwa zaidi ya mwaka mmoja kutokana na upasuaji wa goti aliofanyiwa mara mbili, atarudi uwanjani kwenye mashindano ya Qatar Open ambayo yataanza Machi 8.

Mchezaji tenisi nyota, ambaye ana ubingwa 20 wa Grand Slam katika taaluma yake, hatashiriki Miami Open na badala yake, ataendelea na mazoezi yake kwa muda baada ya Qatar Open.

Akishika nambari 5 katika orodha ya wanaume pekee, Federer alionekana mara mwisho uwanjani kwenye mechi iliyochezwa Januari 30, wakati aliposhindwa na Novak Djokovic kwenye nusu fainali ya Australia Open mwaka jana.Habari Zinazohusiana