Juventus yaponea chupuchupu dakika za majeruhi

Cristiano Ronaldo aikoa Juventus dakika za majeruhi, na kufanikiwa kuvunja rekodi yake mwenyewe

Juventus yaponea chupuchupu dakika za majeruhi

Mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya kombe la Italia umezikutanisha timu za Milan na Juventus. Mchezo huo umemalizika kwa timu hizo kutoka sare ya goli 1-1.

Cristiano Ronaldo amefanikiwa kuvunja rekodi yake mwenyewe kwa kufanikiwa kupachika goli katika michezo 11 mfululizo.

Milan ndio waliokuwa wa kwanza kupata goli, mnamo dk ya 63 kupitia kwa Rebic, huku Juventus ilipata goli la kusawazisha kupitia kwa Ronaldo mnamo dk 90+1 kwa mkwaju wa penati.Habari Zinazohusiana