Habari za kusikitisha kwa mashabiki wa Barcelona

Kufuatia majeraha ya kisigino aliyoyapata wakati wa mazoezi, Dembele amefanyiwa upasuaji na hatoshuka dimbani kwa kipindi cha miezi 6

Habari za kusikitisha kwa mashabiki wa Barcelona

Nyota wa Ufaransa na klabu ya Barcelona, Ousmane Dembele,  ambaye alijeruhiwa kisigino wakati wa mazoezi mnamo Februari 3, amefanyiwa upasuaji kwa mafanikio nchini Finlandia.

Baada ya upasuaji Dembele anatarajiwa kupona kabisa katika kipindi cha  miezi 6. Hiyo inamaanisha kwamba nyota huyo hataonekana tena uwanjani katika msimu huu.

 Habari Zinazohusiana