King Messi!! Mfalme

Usiku wa Tarehe 2.12.2019 utabaki wa kihistoria katika ulimwengu wa soka

King Messi!! Mfalme

Usiku wa Tarehe 2.12.2019 utabaki wa kihistoria katika ulmwengu wa soka, ambapo wapenzi wa mchezo huo walishuhudia Lionel Messi akijinyakulia tuzo ya Ballon D'or kwa mara ya sita.

Leo Messi anakua ndiye mchezaji wa kwanza katika historia ya soka kutwaa taji hilo kwa mara sita huku akimpiku mpinzani wake wa asili, Christiano Ronaldo ambaye ametwaa taji hilo mara 5.

Nyota huyo wa barcelona alikua kwenye mchuano mkali na nyota wa Liverpool, Virgil Van Dijk ambaye ametwaa  Goal 50 player of the year na mchezaji bora wa ligi ya Uingereza.

Licha ya kuifikisha fainali timu yake ya taifa, Van Dijk aliisaidia klabu yake ya  Liverpool kutinga fainali ya champions ligi kwa kuitwanga Barcelona katika mechi ya kihistoria na baadaye kutwaa taji hilo walipocheza fainali dhidi ya Tottenham.

Lakini Leo Messi yeye ameonesha uwezo binafsi mkubwa sana  baada ya kuifungia barcelona magoli 41 katika michezo 44 aloichezea Barcelona na ameongeza.

Messi amekua ni mchezaji wa pekee aliyeweza kufikia kiwango cha magari 40 au 50 kwa kila msimu kwa misimu 11 iliyopita. 

Kwa sasa Lionel Messi ana miaka 32,  na anaonekana kuendelea kuwa tishio katika soka.Habari Zinazohusiana