Leo Katika Magazeti ya Uturuki

Mukhtasari wa Magazeti ya Uturuki 07.06.2021

1652896
Leo Katika Magazeti ya Uturuki

Hürriyet "Rais Erdoğan atangaza! Pigo kubwa kwa shirika la kigaidi"

Rais Recep Tayyip Erdoğan alitangaza kwenye akaunti yake ya Twitter mafanikio ya operesheni ya Shirika la Kitaifa la Ujasusi, ambapo kiongozi mwandamizi wa shirika la kigaidi la PKK na Afisa Mkuu wa Mahmur (Kaskazini mwa Iraq) Selman Bozkır, aliangamizwa.

 

Star "Akar: Jeshi la Wanamaji la Uturuki lilivunja rekodi ya muda wote"

Waziri wa Ulinzi wa Kitaifa Hulusi Akar alisema, "Jeshi la Wanamaji la Uturuki lilivunja rekodi ya muda wote kwa kusafiri kwa masaa 200,000/mwaka. Wameandika ukurasa mpya katika historia ya Vikosi vya Jeshi la Wanamaji na kuongeza mafanikio mpya."

 

Sabah "Ina kinga bora zaidi ya makomborora"

Rais wa Sekta ya Viwanda vya Ulinzi İsmail Demir, alitoa ujumbe kwenye akaunti yake ya mitandao ya kijamii; Uzalishaji mkubwa wa vifurushi vya silaha ziliotengenezwa kwa mizinga ya Leopard 2A4 umeanza na ujumuishaji wake kwenye matangi. "Kifurushi cha silaha kina kinga bora zaidi ya makombora na inayotumika hivi sasa katika mizinga ya Leopard 2A4 katika majeshi ya ulimwengu."

 

Habertürk "Pakdemirli: Mauzo yetu ya samaki yalifikia bilioni 1 na milioni 63"

Waziri wa Kilimo na Misitu Bekir Pakdemirli alisema kuwa mnamo mwaka 2020, uzalishaji wa bidhaa za samaki ulifikia kiwango cha tani 785,000 na sekta hiyo ilifanya mauzo ya nje ya dola bilioni 1 na milioni 63.

 

Yeni Şafak "Rekodi ya miezi 15 ya THY"

Shirika la usafiri wa anga la ndege la Uturuk  lililotekeleza safari za ndege nyingi zaidi kwenye anga ya Ulaya katika miezi 5 ya kwanza ya mwaka 2021, lilifikia idadi kubwa zaidi ya safari za kila siku katika miezi 15 iliyopita kwa jumla ya safari za ndege 863 siku ya Ijumaa.Habari Zinazohusiana