Leo Katika Magazeti ya Uturuki

Mukhtasari wa Magazeti ya Uturuki 27.05.2021

1646452
Leo Katika Magazeti ya Uturuki

Haber Türk: "Tunapanga kurusha ndege yetu ya kivita mwaka 2023"

Mwenyekiti wa Chama cha Haki na Maendeleo (AK Party), Recep Tayyip Erdoğan, alitoa hotuba yake hapo jana kwenye mkutano wa kikundi cha chama chake katika Bunge Kuu la Uturuki na kusema: "Tunapanga kurusha ndege yetu ya kivita isiyokuwa na rubani angani mwaka 2023."

 

Sabah: "Waziri Çavuşoğlu anaenda Ugiriki"

Waziri wa Mambo ya Nje Mevlüt Çavuşoğlu alisema katika taarifa yake hapo jana kabla ya mkutano wa kikundi cha chama chake kwamba atakwenda Ugiriki siku ya Jumatatu, Mei 31. Çavuşoğlu atatembelea mji mkuu wa Athens na Thessaloniki ndani ya wigo wa ziara yake.

 

Yeni Şafak: "Vifaa 5 vya mitambo ya kusafisha vilipuzi kutoka Wizara ya Ulinzi ya Kitaifa kwenda Azerbaijan"

Katika taarifa iliyotolewa jana na Wizara ya Ulinzi ya Kitaifa, ilielezwa kuwa vifaa 5 vya mitambo ya kusafisha vilipuzi (MEMATT) vilivyotengenezwa na Kiwanda cha Jeshi na Shirika la Operesheni ya Meli (ASFAT), ambayo iko chini ya Wizara hiyo, viliwasilishwa Azerbaijan.

 

Vatan: "Chanjo mpya ya BioNTech yaletwa Uturuki"

Ndege iliyobeba shehena ya kwanza ya dozi milioni 120 za chanjo ya Pfizer / BioNTech, ambayo Waziri wa Afya Fahrettin Koca alikuwa ametangaza makubaliano yake hapo awali, ilitua jana katika mji mkuu wa Ankara. Dozi za chanjo zilisafirishwa kwenda kwa Wizara ya Afya na Bohari ya Dawa na malori maalum ya uhifadhi wa baridi.

 

Star: "Yatengenezwa Uturuki, na kuonjwa katika nchi 40"

Katika kipindi cha Januari-Aprili cha mwaka 2021, asali ilisafirishwa kwenda nchi 40 ikiwa ni pamoja na Marekani, Ujerumani, Kuwait na Ubelgiji kwa kiwango cha jumla ya dola milioni 9 elfu 542 na 306.Habari Zinazohusiana