Leo Katika Magazeti ya Uturuki

Leo Katika Magazeti ya Uturuki

1401727
Leo Katika Magazeti ya Uturuki

Hürriyet " Rais Erdoğan azungumza na rais Trump "

Recep Tayyıp Erdoğan , rais wa Uturuki azungumza kwa njia ya simu  na rais wa Marekani kuhusu ushirikiano wa kiuchumi katika kupambana  dhidi ya virusi vya corona. Mkurugenzi  katika kitengo kinachhusika na upashaji habari ikulu ya rais mjini Ankara amesema kwamba viongozi hao wamejadili kuhusu ushirikiano katika mapambano dhidi ya virusi vya corona na kuonesha zaidi  mshikamano miongoni mwa  wanachama wa   Muungano wa kujihami NATO. Ushirikiano kuhusu hali inayoendelea katika ukanda umejadiliwa  kati ya marais hao wawili.

Vatan " dawa dhidi ya virusi vya corona"

Wizara ya ulinzi ya Uturuki  na  afya kuanza mradi utakaopelekea  kutengenezwa kwa dawa dhşdş ya virusi vya corona. Utafiti wa AR-Ge tayari umeanza  na kutumiwa na vimelea ambavyo vatapelekea kufikia malengo. Mradi huo umewasilishwa TUBITAK imefahamisha wizara .

Yenişafak " Uhispania yatoa shukrani kwa Uturuki"

Muimbaji wa Uhispania anaejulikana kwa jina la  Monica Molina  ni miongoni mwa watu waliotoa shukrani kwa Uturuki kwa kujitolea msaada  wa vifaa vya matibabu na madawa nchini Uhispania katika juhudi za kupambana na virusi vya corona. Msanii huyo amesema kuwa  Uturuki imeonesha moyo wake wa ubinadamu katika kipindi hiki kigumu.

Star "Uingereza :   tunasubiri ushirikiano na msaada mwingine kutoka Uturuki"

kutokana na jamga la virusi vya corona  na kupungua kwa  wauguzzi, Uturuki imejitolewa kwa kutoa msaada wa vifaa vya matibabu na madawa katika mataifa Ulaya ikiwemo Uimgereza , Italia na Uhispania.  Waziri Robert Jenrick  amesema kuwa  vifaa ya kujlinda na maambukizi ya korona vinataraji zaidi ya  400 000.Habari Zinazohusiana