Leo Katika Magazeti ya Kimataifa

Mukhtasari wa Magazeti ya Kimataifa 03.06.2021

1650742
Leo Katika Magazeti ya Kimataifa

zdf.de: Mishahara ya wafanyikazi wa nyumbani wauguzi itaongezeka nchini Ujerumani.

Süddeutsche Zeitung: Maombi ya kipaumbele ya chanjo dhidi ya corona (Covid-19) nchini Ujerumani inaisha tarehe 7 Juni.

Deutsche Welle: Shirika la Kazi Duniani (ILO) liliripoti kuwa zaidi ya wafanyikazi milioni 100 ulimwenguni walisukumwa katika umaskini kwa sababu ya mlipuko wa Covid-19.

 

al-Dustur (Jarida la Jordan): Baadhi ya washiriki wa Baraza la Seneti la Marekani walitaka misaada iruhusiwe kuingia Gaza.

al-Quds al-Arabi (Jarida la Kiarabu - Uingereza): "Jeshi linaloua wanawake" ... Hadithi ya kutisha ya mashujaa 39 huko Gaza.

al-Raye al-Qatariyye (Jarida la Qatar): Uturuki na Qatar zimeunganishwa na uhusiano thabiti wa taasisi.

 

Le Monde: Kiongozi wa upinzaji wa Israeli Yair Lapid alitangaza kwamba ameunda umoja wa serikali.

Le Figaro: Mitandao ya kijamii ndio kituo jipya cha biashara ya dawa za kulevya.

France 24: Nambari za dharura nchini Ufaransa zilikuwa nje ya huduma kwa muda kwa sababu ya utendajikazi wa Orange ambaye ni mhusika wa utoaji huduma.

 

El País (Uhispania): Ufaransa itatoa chanjo kwa vijana kati ya umri wa miaka 12 hadi 18 kufikia Juni 15.

Infobae (Argentina): (Akijitangaza Rais wa mpito nchini Venezuela) Juan Guaidó alaani kukamatwa kwa kiongozi wa upinzaji wa Nicaragua Cristiana Chamorro.

Telesur (Venezuela): Kamati ya Ukosefu wa Ajira ilitangaza uhamasishaji mpya baada ya kukutana na Serikali ya Colombia ambayo haikuweza kufikia makubaliano.

 

Lenta.ru: Kulingana na tafiti zilizofanywa nchini Urusi, idadi kubwa ya watu iko tayari kulipa ushuru mkubwa mradi serikali inatoa msaada zaidi kwa raia wa kipato cha chini.

RBK: Shughuli za wawekezaji wa kigeni nchini Urusi zilipungua hadi kiwango cha 2014.

TASS: Waziri wa Afya wa Urusi Mikhail Murashko alisema kuwa hakuna wimbi la tatu katika janga la Covid-19 nchini Urusi, na kwamba idadi ya kesi za maambukizi ilipungua katika mikoa yote ya nchi.

 Habari Zinazohusiana