Leo Katika Magazeti ya Kimataifa

Mukhtasari wa Magazeti ya Kimataifa 27.01.2021

1571848
Leo Katika Magazeti ya Kimataifa

Le Parisien: Kocha Msaidizi wa Başakşehir Pierre Webo, ambaye alikumbwa na shambulizi la ubaguzi wa rangi katika mechi dhidi ya Paris Saint Germain mwezi uliopita, amelezea masikitiko yake ya kukosa kuungwaji mkono vya kutosha na kocha wa zamani wa PSG Thomas Tuchel.

Le Monde: Covid-19 – EU yaonya watengenezaji wa chanjo kuhusu 'majukumu' yao.

France 24: Covid-19 - Waalimu, wanafunzi na wauguzi wa shule nchini Ufaransa wafanya mgomo (kupinga sera ya serikali ya kupambana na janga).

 

al-Quds al-Arabi (Gazeti la Kiarabu - Kiingereza): Washington (utawala): Tunaunga mkono suluhisho la serikali mbili (huko Palestina) na tunataka uhalalishaji zaidi na Israel.

al-Raye al-Qatariyye (Gazeti la Qatar): Amiri Mkuu wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamed Al-Sani alituma ujumbe wa pole kwa Mfalme wa Saudi Arabia, Salman bin Abdulaziz, kufuatia kifo cha Mwanamalkia Tarfe binti Saud bin Abdulaziz.

al-Düstur (Gazeti la Jordan): (Katibu Mkuu wa UN Antonio) Guterres: Ulimwengu upo kwenye shida mbaya zaidi ya kiuchumi katika karne.

 

Deutsche Welle: Mabadiliko mapya yamesababisha hali ya wasiwasi nchini Ujerumani: Janga hilo haliwezi kudhibitiwa katika kipindi hiki cha hali ya hewa ya joto.

Süddeutsche Zeitung: Simu ya kwanza ya (Waziri Mkuu wa Ujerumani Angela) Merkel na (Rais wa Marekani Joe) Biden: Matarajio ya Berlin ni makubwa.

Bild.de: Mabadiliko ya Corona: Waziri Mkuu wa Ujerumani Angela Merkel ataka vizuizi vya usafiri!

 

El Mundo (Uhispania): Kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi ambao hawawezi kuhudhuria madarasa ya kawaida kwa sababu ya Covid-19 kumezuwa hali ya wasiwasi kwa walimu na wazazi: Idadi ya madarasa katika karantini imeongezeka kwa asilimia 60.

La Vanguardia (Uhispania): Kiwango cha ukuaji wa Uhispania kitashuka chini zaidi kuliko ilivyotarajiwa katika miaka ijayo kulingana na utabiri wa Shirika la Fedha la Kimataifa.

Telesur (Venezuela): Rais wa Venezuela Nicolás Maduro alitangaza wiki hii kuwa utengenezaji wa dawa ya asili ya Carvativir kwa ajili ya matibabu ya corona ulianza.

 

Kommersant: Rais wa Urusi Vladimir Putin alipigiwa simu ya kwanza na Rais mpya wa Marekani Joe Biden.

RIA Novosti: Rais wa Urusi Vladimir Putin aliwasilisha uamuzi wa kupanua Mkataba Mpya wa Mkakati wa Kupunguza Silaha (New START) kwa Duma, mrengo wa chini wa bunge la Urusi.

TASS: Urusi imeanza tena safari za ndege za kawaida katika nchi za Vietnam, India, Finland na Qatar, ambazo zilisitishwa kwa sababu ya janga mwaka jana.Habari Zinazohusiana