Zawadi ya gari kwenye kampeni ya chanjo Urusi

Urusi kutoa zawadi ya gari kwenye kampeni ya chanjo iliyozinduliwa dhidi ya corona (Covid-19)

1657065
Zawadi ya gari kwenye kampeni ya chanjo Urusi

Zawadi ya gari itatolewa katika kampeni ya chanjo iliyozinduliwa dhidi ya corona (Covid-19) huko Moscow, mji mkuu wa Urusi.

Katika taarifa iliyoandikwa, Meya wa Moscow Sergey Sobyanin alikumbusha kwamba hatua dhidi ya janga hilo zimeanzishwa tena.

Akisisitiza kuwa mchakato wa chanjo dhidi ya Covid-19 unapaswa kuharakishwa ili kuepukana na tahadhari mpya, Sobyanin alitangaza kwamba walianzisha kampeni ya chanjo kwa raia walio na umri wa zaidi ya miaka 18.

Sobyanin alisema,

"kati ya Juni 14-Julai 11, wale ambao watapewa dozi yao ya kwanza ya chanjo watashiriki katika mchezo wa bahati nasibu kwa ajili ya zawadi ya gari. Kila wiki, michezo 5 ya bahati nasibu ya zawadi ya gari itafanyika, ambayo ina thamani ya takriban rubles milioni 1 (takriban dola elfu 14)."

Akikumbusha kwamba alichomwa chanjo mnamo Mei 2020, Sobyanin alibainisha kupokea chanjo ya "Sputnik V" kwa mara nyingine tena siku mbili zilizopita.Habari Zinazohusiana