Shambulizi la bomu katika shule Afghanistan

25 wafariki kwenye shambulizi la bomu lililotekelezwa mbele ya shule katika mji mkuu wa Kabul nchini Afghanistan

1636581
Shambulizi la bomu katika shule Afghanistan

Watu 25 walipoteza maisha kwenye shambulizi la bomu lililotokea mbele ya shule katika mji mkuu wa  Kabul nchini Afghanistan.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani Tarik Aryen alisema katika taarifa yake aliyotoa kwa waandishi wa habari kwamba shambulizi la bomu lilitekelezwa mbele ya Shule ya Seyid-u heduheda katika eneo la Dasht-i Barchi mjini Kabul.

Akibainisha kuwa raia 25 walipoteza maisha katika shambulizi hilo kulingana na taarifa za awali, Aryen alisema kuwa raia wengine 52 walijeruhiwa na walikuwa na wasiwasi juu ya ongezeko la idadi ya vifo.

Mashuhuda wa tukio walidai kuwa mshambuliaji alilenga mlango wa kuingilia wa shule hiyo kwa kutumia gari lililosheheni bomu, na kwamba zaidi ya raia 30 waliuawa katika shambulizi hilo.

Barabara zote zinazoelekea eneo la shambulizi zilifungwa kwa muda.

Hakuna mtu aliyedai kuhusika na shambulizi hilo hadi kufikia sasa.

Kwa upande mwingine, Taliban walitangaza kwamba hawakuwa na uhusiano wowote na shambulizi hilo, na walilaani utekelezwaji wa shambulizi.Habari Zinazohusiana