Kazakhstan kutuma misaada Kyrgyzstan

Kazakhstan yatangaza mpango wa kutuma misaada ya kibinadamu kwa Kyrgyzstan.

1636233
Kazakhstan kutuma misaada Kyrgyzstan

Kazakhstan itatuma misaada ya kibinadamu kwa Kyrgyzstan.

Msemaji wa Rais wa Kazakhstan Berik Uali alitoa taarifa kwenye mitandao ya kijamii na kusema kwamba Rais Kasım Cömert Tokayev ameamua kupeleka misaada ya kibinadamu Kyrgyzstan kwa niaba ya watu wa nchi hiyo.

Katika taarifa hiyo, ilibainika kuwa tani elfu 10 za unga wa ngano zitatumwa kama sehemu ya misaada ya kibinadamu kwa Kyrgyzstan kulingana na kanuni za kuzingatia undugu, urafiki na ushirikiano wa kimkakati, na kwamba serikali ya Kazakhstan imeanzisha juhudi za kutekeleza misaada hiyo.

Tokayev, ambaye alizungumza kwa simu na mwenzake wa Kyrgyz Sadır Caparov baada ya mzozo wa kijeshi uliofanyika kwenye mpaka wa Kyrgyzstan-Tajikistan mnamo Aprili 29, alisema kuwa wako tayari kutoa misaada ya kibinadamu kwa Kyrgyzstan.Habari Zinazohusiana