Mafuta kutoka Iran kwenda Syria

Iran yaendelea kutuma mafuta Syria

1633015
Mafuta kutoka Iran kwenda Syria

Mapipa milioni 1.5 ya mafuta yasiyosafishwa yaliyotumwa kutoka Iran yanatarajiwa kuwasili katika mji wa bandari wa Baniyas nchini Syria wiki hii.

Kulingana na taarifa kwenye akaunti ya Twitter ya mfumo wa ufuatiliaji wa meli za kimataifa Tanker Trackers, Iran inaendelea kusafirisha mafuta yasiyosafishwa kwenda Syria.

Mwezi uliopita, Iran ilisafirisha mapipa zaidi ya milioni 3 ya mafuta kusuluhisha katika mikoa iliyo chini ya utawala wa Bashar al-Assad.


Tagi: #mafuta , #Iran , #Syria

Habari Zinazohusiana