Uchaguzi mkuu kufanyika Peru

Wananchi wa Peru kupiga kura hapo kesho kwenye uchaguzi mkuu ili kumchagua rais na wawakilishi wa bunge

1618937
Uchaguzi mkuu kufanyika Peru

Nchi ya Peru iliyoko Amerika ya Kusini, inaelekea kwenye uchaguzi utakaofanyika hapo kesho ili kumchagua rais atakayehudumu hadi mwaka 2026.

Katika uchaguzi huo, ambapo wagombea 18 watashindana nchini Peru na zaidi ya watu milioni 25 watajitokeza kupiga kura katika duru ya kwanza, wabunge 5 watachaguliwa kwa Bunge la Andes, ambalo ni sehemu muhimu ya nchi, na wawakilishi 130 wa Bunge pamoja na rais watabainishwa.

Wagombea wanatakiwa wapate asilimia 50 ya kura halali ili kushinda kiti cha urais katika duru ya kwanza. Vinginevyo, wagombea wawili walio na kura nyingi zaidi watashindana katika duru ya pili itakayofanyika Juni 6.

Kulingana na utafiti wa hivi karibuni nchini, mgombea wa upande wa kulia  Yonhy Lescano, mgombea wa mrengo wa kushoto Veronika Mendoza na mgombea wa mrengo wa kulia Hernando de Soto wanaonekana kama wagombea walio na idadi kubwa ya kura katika duru ya kwanza.

Hakuna mgombea anayetarajiwa kushinda kinyang'anyiro cha urais katika duru ya kwanza kulingana na kura za maoni.Habari Zinazohusiana