Dozi za Covid-19 zapunguza idadi ya wagonjwa wa kulazwa hospitalini

Dozi ya Pfizer-BioNTech na Oxford-AstraZeneca ya corona (Covid-19) yapunguza wagonjwa wa kulazwa kwa zaidi ya asilimia 80

1593651
Dozi za Covid-19 zapunguza idadi ya wagonjwa wa kulazwa hospitalini

Dozi moja ya chanjo ya Pfizer-BioNTech na Oxford-AstraZeneca ya corona (Covid-19) iliripotiwa kuwa imepunguza kulazwa kwa zaidi ya asilimia 80 ya wagonjwa.

Shirika la Afya ya Umma la Uingereza lilichapisha matokeo ya kwanza juu ya athari za chanjo ya Pfizer-BioNTech na Oxford-AstraZeneca katika kupunguza maambukizo ya Covid-19.

Kulingana na rmatokeo ya wiki 4 baada ya chanjo hiyo, ilionekana kuwa dozi moja ya chanjo ya Pfizer-BioNTech ilikuwa na ufanisi wa asilimia 57-61 wa kinga dhidi ya Covid-19, na chanjo ya Oxford-AstraZeneca ilikuwa na ufanisi wa asilimia 60-73.

Imefahamishwa kuwa dozi moja ya chanjo zote mbili ilikuwa na ufanisi zaidi ya asilimia 80 katika kuzuia kulazwa kwa wagonjwa wenye umri wa miaka 80 na zaidi hospitalini wiki 3-4 baada ya chanjo. Uthibitisho huo pia ulionyesha kuwa chanjo ya Pfizer ilipunguza idadi ya vifo vinavyotokana na Covid-19 kwa asilimia 83.

Waziri wa Afya Matt Hancock, alitoa taarifa kwenye mkutano na waandishi wa habari, na kuelezea maoni yake kwamba matokeo hayo yalikuwa "yenye nguvu sana", na kubainisha kuwa chanjo zinaonekana kusaidia kupunguza shinikizo kwa hospitali na kuokoa maisha.

Aina mpya ya virusi vya Covid-19 inayoenea kwa kasi na kuwa hatari zaidi,  ilisababisha ongezeko la vifo na maambukizi Uingereza.

Walakini, hatua za karantini na athari ya chanjo iliyoanza Januari 5, zimeweza kupunguza kesi za kila siku hadi chini ya elfu 10 na vifo hadi chini ya 500 katika wiki za hivi karibuni.Habari Zinazohusiana