Ngozi Okonjo-Iweala aonya kuhusu ubaguzi katika usambazaji wa chanjo

Ngozi Okonjo-Iweala, Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Biashara Ulimwenguni (WTO), ameonya dhidi ya "ubaguzi"

1585312
Ngozi Okonjo-Iweala aonya kuhusu ubaguzi katika usambazaji wa chanjo

Ngozi Okonjo-Iweala, Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Biashara Ulimwenguni (WTO), ameonya dhidi ya "ubaguzi" katika usambazaji wa chanjo dhidi ya corona.

Okonjo-Iweala ambaye hapo awali alikuwa Kiongozi wa Chama cha Chanjo Duniani (GAVI)
ameiambia BBC, 

"Wakati nchi tajiri zikiwapatia chanjo raia wao, nchi masikini hazipaswi kusubiri chanjo." 

Okonjo-Iweala amesema kuwa katika wiki za hivi karibuni, nchi nyingi zimekuwa zikijaribu kuzuia usafirishaji wa chanjo zinazotengenezwa ndani ya mipaka yao, na kubainisha kuwa hali hii itazuia ahueni ya ulimwengu. 

"Hakuna nchi inayoweza kujisikia salama ikiwa kila nchi itafikiria watu wake.", alisema.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Guterres pia amezitaka nchi zote kuwa na 'mshikamano' na kuondoa 'utaifa wa chanjo' kwa kuunga mkono chanjo kwa watu wote.

 Habari Zinazohusiana