Operesheni dhidi ya Taliban yapelekea vifo vya watu 12 Afghanistan
Imeripotiwa kuwa raia 12 wameuawa katika operesheni ya Kikosi cha Anga cha Afghanistan

Imeripotiwa kuwa raia 12 wameuawa katika operesheni ya Kikosi cha Anga cha Afghanistan dhidi ya Taliban katika mkoa wa Nimruz magharibi mwa Afghanistan.
Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Nimruz, Baz Muhammed Nasser, amewaambia waandishi wa habari kwamba Vikosi vya Anga vya Afghanistan vilifanya shambulizi la anga dhidi ya Taliban katika mkoa wa Manzari wa wilaya ya Hasrud ya Nimruz.
Nasır amesema kuwa raia 12 walipoteza maisha na raia 2 walijeruhiwa kutokana na bomu kugonga nyumba wakati wa operesheni hiyo.
Msemaji wa Gavana wa Nimruz Rahmatullah Ömeri amebainisha kuwa tukio hilo linachunguzwa.
Habari Zinazohusiana

Ajali ya treni ya abiria Pakistan
Mmoja afariki, 40 wajeruhiwa kwenye ajali ya treni ya abiria iliyotokea nchini Pakistan

Palestina kununua chanjo ya Covid-19 kutoka China
Palestina yasaini makubaliano na China kwa ajili ya ununuzi wa chanjo ya Sinovac dhidi ya Covid-19