Shambulizi la Taliban

Polisi watano wamepoteza maisha katika shambulizi la silaha la wanamgambo wa Taliban

1489632
Shambulizi la Taliban

Polisi watano wamepoteza maisha katika shambulizi la silaha la wanamgambo wa Taliban katika wilaya ya Tegab mkoa wa Kapisa nchini Afghanistan.

Msemaji wa Idara ya Polisi ya Kapisa Abdul Şayık Şuriş amesema kuwa wanamgambo hao walifanya shambulizi la silaha katika kituo cha wilaya ya Tegab.

Akisema kuwa maafisa 5 wa polisi wamepoteza maisha katika shambulizi hilo, Şuriş amesema kuwa walinzi 7 wamejeruhiwa.

Shuriş amebainisha kuwa wanamgambo wa Taliban pia walipoteza maisha katika mapigano yaliyofuatia shambulizi hilo.

Kwa kuongezea, Wizara ya Ulinzi ya Afghanistan imetangaza kuwa wanamgambo wa Taliban wamefanya mashambulizi katika majimbo 15 ya nchi hiyo katika masaa 24 yaliyopita.Habari Zinazohusiana