Mgodi wa marumaru waporomoka Pakistan

Wachimbaji 22 wamepoteza maisha yao kutokana na kuporomoka kwa mgodi wa marumaru kaskazini magharibi mwa Pakistan.

1487874
Mgodi wa marumaru waporomoka Pakistan

Wachimbaji 22 wamepoteza maisha yao kutokana na kuporomoka kwa mgodi wa marumaru kaskazini magharibi mwa Pakistan.

Kulingana na habari kwenye wavuti ya Dawn, maafisa wameripoti kuwa mgodi wa marumaru uliokuwa na wafanyakazi zaidi ya 30 umeanguka katika mji wa Mohmand, jimbo la Khyber Pakhtunkhwa.

Shughuli ya uokoaji zinaendelea.

Kuna wasiwasi ya kuwa huenda idadi ya waliopoteza maisha ikaongezeka.

Uchunguzi rasmi umeanzishwa kwani sababu kuu ya kuporomoka kwa mgodi huo haijajulikana bado.

 Habari Zinazohusiana