Shambulizi la silaha Afghanistan

Maafisa Usalama wanne wamepoteza maisha katika shambulizi la silaha lililofanywa na wanamgambo wa Taliban

1479713
Shambulizi la silaha Afghanistan

Maafisa Usalama wanne wamepoteza maisha katika shambulizi la silaha lililofanywa na wanamgambo wa Taliban katika kituo cha jeshi katika mkoa wa Nangarhar mashariki mwa Afghanistan.

Msemaji wa Nangarhar Ataullah Hogyani amesema kuwa shambulizi hilo limefanywa dhidi ya kituo cha wanajeshi katika wilaya ya Hogyani.

Imeripotiwa kuwa watu wanne wamepoteza maisha na wengine nane wamejeruhiwa.

Hata hivyo, kulingana na taarifa ya msemaji wa Gavana wa eneo hilo, Taliban nao walishambuliwa na kupoteza wanamgambo wao kumi na tatu na wengine watatu kujeruhiwa.

Taliban nao wametoa ripoti yao binafsi inayoonyesha kuwa maafisa usalama 19 wameuawa katika shambulizi hilo.Habari Zinazohusiana