Ardhi ya Anatolia  yaonesha ulimwenguni ni maana ya  udugu

Mkurugenzi w akitengo cha mawasiliano ikulu asema kwamba ardhi ya Anatolia imeonesha ulimwengu mzima nini maanaua udugu

1466491
Ardhi ya Anatolia  yaonesha ulimwenguni ni maana ya  udugu


Mkurugenzi w akitengo cha mawasiliano ikulu asema kwamba ardhi ya Anatolia imeonesha ulimwengu mzima nini maanaua udugu.

Fahrettin Alun, mkurugenzi katika kitengo kinachohusika na mawasiliano ikulu ya rais mjini Ankara amesema kwamba ardhi ya Anatolia imeonesha uliöwengu mzima nini maana ya udugu.

Ardhi ya Anatolia ni ardhi ambay ina utofauti wa kila aina ikiwa pamoja na utofauti wa imani, makabila, lugha   na hili ni tangu zama za kale.

Altun amesema kwamba ardhi hiyo watu kutoka katika jamii na tamduni tofauti wameishi kwa amani kwa muda wa miaka dahari licha ya kuwa na utofauti hiyo.

Katika ujumbe wake aliopeperusha upitia ukurasa wake wa Twitter, mkurugenzi huyo ameambatanisha video ambayo inasimulia historia  kwa ufupi ya Anatolia na utamaduni wake  ambao  watu katika jamii ya waislamu, wayahudi, waarmenia, waasyrian na wagiriki waliishi pamoja kwa amani kwa muda mrefu.

Kuhani wa kanisa katoliki Antalya Domomenico Bertogi  amesema kupitia video hiyo kuwa amekuwa akiishi katika  kitongoji kimoja ambacho wakazi wake wengi ni waislamu wa dhehebu la sunni bila ya tataizo la aina yeyote lile.

Kuhani huyo amesema  kuwa , katika kitongoji hicho watu wanaishi kama ndugu na hautoona tofauti yeyeote.

Kiongozi mwingine wa kidini Harun Jamal amesema kuwa majumba ya ibada Antakya ikiwa ni masinangogi , makanisa na misikiti  yapo  pamoja.
 Habari Zinazohusiana