Viongozi waliothirika na maambukizi ya virusi vya corona ulimwenguni

Hakuna mtu alienusurika na maambukizi y virusi vya corona kutokana na wadhifa wake

1452617
Viongozi waliothirika na maambukizi ya virusi vya corona ulimwenguni


Virusi vya corona  baada ya kuanza katika jimbo la Wuhan nchini China mwishoni mwa mwaka  2019   na kuenea ulimwenguni kote hakuna mtu ambae angejinasibu kuwa yupo salama na maambukizi.

Baada ya kuenea katika mataifa tofauti ulimwenguni  viongozi tofauti wa ngazi za juu pia walijipata wamekuwa waathirika wa covid-19.

Rais Brazil Jair Bolsonaro alitajwa kuwa amepimwa na kugunduliwa kuwa na maambukizi  ya virusi vya corona.

Tangu kuanza  kwa janga hilo, nchini China viongozi tofauti wamegunduliwa kuwa na maambukizi ya covid-19 wakiwemo mawaziri na wabunge.

Nchini Uingereza, waziri mkuu mpya Boris Johnson , waziri wa Urusi  Mihail Mishustin, waziri mkuu wa Armenia Nikol Pahinyan na waziri wa Guinea Bissaeu Nuno Gomes Nabiam ni viongozi ambao waliambukiwa virusi hivyo hatari.

Nchini Iran,  makamu wa rais Masume IBtikar, naibu waziri wa ulinzi wa Sudan Kusini , Carmen Calvo  wa uhispania pia walipmwa na kugunduliwa kuwa na maambukizi ya  corona.
 Waziri wa afya wa Uingereza  Matthew Hancock, waziri wa afya wa Israel Yaakov Litzman, waziri wa afya wa Afghanistan Firuziddin Firuz, waziri wa afya wa Ghana Kwaku Agyemang-Manu, waziri wa mambo ya ndani wa mambo ya ndani wa Australia  Peter Dutton, waziri  wa utamaduni wa Ufaransa  Franck Riester, waziri wa utamaduni wa Ufaransa Olga Lyubimova, waziri wa mmazingira wa Poland   Michael Wos  walifanyiwa vipimo vya virusi vya corona.Habari Zinazohusiana