Uturuki yakemea shambulizi dhidi ya sanamu la Baba wa taifa Mustafa Kemal Atatürk Marekani

Serikali ya Uturuki imekemea vikali shambulizi dhidi ya sanamu la Baba wa taifa Mustafa Kemal Atatürk mjini Washington

1445985
Uturuki yakemea shambulizi dhidi ya sanamu la Baba wa taifa Mustafa Kemal Atatürk Marekani


Serikali ya Uturuki imekemea vikali shambulizi dhidi ya sanamu la Baba wa taifa Mustafa Kemal Atatürk mjini Washington.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Uturuki  Hami Aksoy  amejibu kwa taarifa ya maandishi  kuhusu  kitambaa cha kufanyia usafi kilichotungikwa  kwenye sanamu la Baba wa taifa Mustafa Kemal Atatürk mjini Washington.

Tukio hilo limetokea mbele ya jengo ambalo kunaptikana ubalozi wa Uturuki mjini Washington nchini  Marekani.

Kitendo hicho kimekemewa vikali.

Aksoy amekumbusha kuwa  Mustafa Kemal Atatürk  ndio muanzilishi wa Jamhuri ya Uturuki  na ni kiongozi muhimu katika Histoira  ulimwenguni.

Taarifa iliotolewa kuhusu tukio hilo imefahamishwa kwamba  ubalozi wa Uturuki mjini humo Washington umewakilisha  ombi lake  kwa mamlaka husika  ili watu walioendesha tukio hilo  wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.Habari Zinazohusiana