Kisa cha kwanza cha maambukizi ya Corona kutoka kwa binadamu kwenda kwa paka charekodiwa

Nchini Ubelgiji mwanamke mmoja aliyekuwa na virusi vya Corona amuambukiza virusi hivyo paka wake, hicho ni kisa cha kwanza cha namna hiyo barani Ulaya.

1386590
Kisa cha kwanza cha maambukizi ya Corona kutoka kwa binadamu kwenda kwa paka charekodiwa

Huko nchini Ubelgiji, mwanamke mmoja aliyekuwa na maambukizi ya virusi vya Corona (Covid-19) amemuambukiza virusi paka wake.

Tukio hilo lililotokea katika mji wa Liege, limerekodiwa kama tukio la kwanza la maambukizi barani Ulaya kutoka kwa binadamu kwenda kwa  paka.

Mamlaka zimeaarifu kwamba hakuna  uthibitisho wowote unaoonyesha kwamba maambukizi yanaweza kutokea kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.

 

 Habari Zinazohusiana