Tafiti juu ya dawa inayotibu virusi vya Corona

Tafiti juu ya dawa au kinga inayoweza kutibu virusi vya Corona

1381531
Tafiti juu ya dawa inayotibu virusi vya Corona

Tafiti juu ya tiba ya virusi vya Corona (Covid-19) zinaendelea huku virusi hivyo vikizidi kuenea dunia nzima.

Mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa bioteknoojia cha nchini China, Zhang Xinmin amesema kwamba utafiti uliofanywa juu ya dawa iliyotengenezwa nchini Japan kwa ajili ya kutibu mafua umeonyesha kwamba dawa hiyo inaweza kuharakisha mgonjwa kupata nafuu.

Dawa hiyo ambayo inaitwa Faviprapir, na pia hujulikana kama Avigan au Favilavir ilitumika kwa kundi la wagonjwa.

Kituo hicho cha utafiti cha nchini china kilitanabainisha kwamba muda wa kupata nafuu ulipungua kutoka siku 11 hadi siku 4 kwa wagonjwa waliotumia tiba ya dawa hio. Asilimia 91 ya wagonjwa walionyesha kuboreka katika afya ya mapafu.

Kwa upande wa shirika la afya duniani limesema kwamba ugunduzi huo ni kitu muhimu katika kufikia tiba ya ugonjwa wa Corona.

Shirika la afya ya jamii la Uingereza limetangaza kwamba linafanyia utafiti juu ya “antibody” itakayoweza kumkinga mtu na maambukizi ya virusi vya  Corona.

Mpaka hivi sasa hakuna kinga wala dawa iliyothibitishwa na kupitishwa kwamba inatibu ugonjwa wa Corona.

 

 Habari Zinazohusiana