Rais Donald Trump azungumza na mwanamfalme mrithi wa Saudia

Rais Donald Trump wa Marekani na mwanamfalme mrithi wa Saudia, Muhammed bin Salman wazungumza kwa njia ya simu

1376604
Rais Donald Trump azungumza na mwanamfalme mrithi wa Saudia

Donald Trump, Rais wa Marekani azungumza kwa njia ya simu na Muhammed bin Salman, mwanamfalme mrithi wa Saudia juu ya masoko ya nishati ulimwenguni.

Msadizi wa msemaji mkuu wa Ikulu ya Marekani, Judd Deere ametoa taarifa ya maandishi, na katika taarifa hiyo amefahamisha juu ya mawasiliano kwa njia ya simu aliyoyafanya Rais Trump na mwanamfalme mrithi.

Katika taarifa yake hiyo Deere alisema,

“Trump amezungumza na mwanamfalme mrithi juu ya soko la nishati ulimwenguni, pamoja na hilo walizungumza pia juu ya masuala  mengine muhimu ya kikanda na mahusiano baina ya mataifa yao mawili”.

Kufuatia kuporomoka kwa soka la hisa la New York siku ya Jumatatu, Rais Trump kupitia ukurasa wake wa Twitter alisema,

“Urusi na Saudia zinazozana juu ya bei na kiwango cha mafuta katika soko,kutokana na hilo na habari za uwongo soko la hisa limeporomoka”.Habari Zinazohusiana