Je wajua moja ya vinywaji vya kale kabisa vya kituruki , Boza, kina faida nyingi kwa afya ?

Bakteria wanaopatikana katika kinywaji cha Boza hukifanya kinywaji hiki kuwa cha "kiprobiyotiki" na kumpa mlaji faida nyingi kiafya

1372083
Je wajua moja ya vinywaji vya kale kabisa vya kituruki , Boza, kina faida nyingi kwa afya ?

 

Boza ni kinywaji cha utamaduni wa kituruki ambacho matumizi yake yalianza maelfu ya miaka iliyopita.

Siku hizi kinywaji hiki pia hutumika katika mataifa ya asia ya kati na yale ilipokuwa dola la Ottomania. Kwa nchini Uturuki Boza ni kinywaji ambacho hutumiwa zaidi katika majira ya baridi kikiambatanishwa na njugu za njano.

Kinywaji hichi hutengenezwa kutokana na unga wa mahindi ya njano ukichanganywa na maji na sukari.

Kinywaji hichi hupendelewa zaidi majira ya baridi.

Katika kinywaji hichi cha Boza ambacho hutengenezwa kwa kuchachishwa wanapatikana bakteria wengi wanaozalisha tindikali ya laktiki. Bakteria hawa hukipa sifa ya “Probiyotiki” kinywaji hichi.

Kutokana na kuwa na bakteria hawa wenye faida kinywaji hichi huimarisha mfumo wa ulinzi wa mwili, na kuongeza kinga ya mwili.

Bakteria wanaopatikana katika kinywaji cha Boza husafisha mwili kutokana na sumu zinazopatikana katika vyakula tunavyokula, pia huondoa visababishi vya mzio na saratani mwilini.

Kwa hakika Boz ni kinywaji chenye lishe ya kutosha na kinachotia nguvu.  Kinywaji hichi kina wanga kwa wingi pamoja na vitamini B.

Ni kwa ajili hiyo kinywaji hichi hupendekezwa kwa wale wanaotaka kuongeza kilo za mwili, kwa vijana wanaokuwa, kwa wagonjwa, kwa wafanyakazi wanaofanya kazi ngumu na kwa wale wanaohitaji lishe yenye nishati ya kutosha.

Kinywaji cha Boza pia kina  virutubisho vifuatavyo kwa wingi vitamin A, B na E na madini ya Kalsiyum, chuma na Phosphurus.

Cha kuzingatia  zaidi ni kwamba kinywaji Boza ni lazima kitengenezwa katika mazingira ya usalama na usafi mkubwa.Habari Zinazohusiana