Erdoğan: "Hatutosahau msaada wa Pakistani  katika vita vya ukombozi"

Rais wa Uturuki   akiwa nchini Pakistani  asema kwamba kamwe Uturuki haitosahau msaada wake katika vita vya ukombozi

Erdoğan: "Hatutosahau msaada wa Pakistani  katika vita vya ukombozi"


Rais wa Uturuki   akiwa nchini Pakistani  asema kwamba kamwe Uturuki haitosahau msaada wake katika vita vya ukombozi.

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan akiwa  katika ziara yake rasmi nchini Pakistani ambapo aliwasili Alkhamis amesema  kuwa kamwe Uturuki haitosahau msaada wa Pakistani  katika kipindi cha vita vya ukombozi.

Katika hotuba yake aliotoa rais Erdoğan ameendelea kufhamisha kuwa  Uturuki itaendelea kushirikiana na Pakistani katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Suala zima kuhusu  Jammu na Kashmir pia limezungumzwa na rais Erdoğan.

Rais Erdoğan amehotubia katika bunge la  Pakistani katika ziara yake hiyo.

Uturuki imepongeza Pakistani kwa kuiunga mkono katika mapambano yake dhidi ya ugaidi  wakati ambapo mataifa yanayojinasibu   kutetea haki za binadamu na demokrasia  wakiwapokea magaidi na kuketi nao katika meza moja.

Rais Erdoğan amezungumza pia  kuhusu hali inayoendelea Idlib nchini Syria.
Madhamuni ya Uturuki Idlib  ni kuzuia mashambulizi dhidi ya watu zaidi ya  milioni 4  , mashambulizi ambayo  yanaendeshwa na  jeshi la Syria.

Kuhusu Libya  na Yemen , rais Erdoğan amesema kuwa  vile vile  malengo ni kuzuia damu za watu wasiokuwa na hatia kuendelea kumwagika.

Mpango wa amani wa rais Trump kuhusu Mashariki ya Kati kati ya Mamlaka ya wapalestina na Israel, rais Erdoğan ameonesha msimamo wake kwa mara nyingine.
 Habari Zinazohusiana