Bara la Afrika na mapambano dhidi ya virusi vya corona

Bara la Afrika na mapambano dhidi ya virusi vya corona

Bara la Afrika na mapambano dhidi ya virusi vya corona


 Wakati ambapo virusi vya corona aina ya (nCoV 2019)  imekuwa kama tishio ulimwenguni, ni baada ya shirika la Umoja wa Mataifa ambalo linahusika na afya  kutangaza kuwa  virusi vya corona imekuwa tishio ulimwenguni.

Taarifa iliotolewa na mamlaka ya China kuhusu virusi hivyo , idadi ya watu waliofariki kutokana na mlipuko wa virusi hivyo ilitangazwa na kuoneakana kuwa ni tukio la kustusha. Idadi ya watu ambao tayari wamekwishaambukiwa na virusi imefikia watu takriban  42200.

Nje ya China  ambapo kuligundulika kwa mara ya kwanza virusi vya corona,  watu wawili  walitangazwa kufariki nchini Ufilipino na Hong Kong.

Watu wengine walitangazwa kupimwa na kukutwa wakiwa na visuri hivyo katika mataifa mengine  24.

Mtafiti Ibrahim Bachir Abdoulaye  mwanafunzi katika kitivo cha dokta katika chuo kikuu cha Bayruth anatuchambulia ...

Licha ya kuwa hadi sasa hakuna mtu yeyote ambae amekutwa na virusi hivyo,  hatari ya kutokea maambukiza kwa haraka ni    kubwa mno.

Jambo hilo linatokana na ukaribu uliopo katika ushirikiano katika  ya mataifa ya bara la Afrika na China.

Bara la Afrika mshirika wake mkubwa katika katika sekta ya biashara ni  China. 

Hofu kubwa ni kutokana na uhaba wa vifaa vya matibabu na ukosefu wa teknolojia ya kisasa katika matibabu.

Ushirikiano uliopo katika sekta ya biashara   kati ya China na mataifa ya bara la Afrika  ni mkubwa na hadi kupelekea  hali ya kuwa na "utegemezi " kwa China. 

Zaidi ya raia wa China milioni 1 wanaishi barani Afrika  huku wakiendesha biashara zao. Tunafahamu kuwa bara la Afrika lina wakazi  ambao wanakadiriwa kuwa  bilioni 1,2.  

Kwa uğpande mwingine waafrika ambao ni wanafunzi 80 000 wapo China wakiendelea na masomo yao, watano miongoni mwao  waanapatikana katka mji wa Wuhan.

Mataifa ya bara la Afrika ,  kama ilivyo katika mataifa mengne ulimwenguni  yamaechukuwa hatua katika uchunguzi katika safari kuelekea nchini China.

Hatua hiyo imechukuliwa bia shaka kwa lengo la kuzuia kuenea kwa virusi.

Licha ya kuwa yapo mataifa ambayo yaneandelea na safari zake kuelekea China kutokana na  biashara, mataifa mengi yamechukuwa hatua ya kusitisha safari zake kuelekea nchini China.

Kwa mfano, shirika  la ndege  la Kenya la , Rwanda, Moroc, Misri, Madagascar , Visiwa vya Mautius na Tanzania  yamesitisha safari zake  kuelekea nchini China.

Baadhi ya mataifa tayari yamechukuwa hatua ya kusitisha utoaji wa visa kwa raia wa China.

Msumbiji ni mfano ulio hai wa mataifa ambayo yamesiirisha utoa visa kwa raia wa China.

Afrika Kusini nayo imechukuwa hatuo kuhusu bidhaa kutoka China , shirika la ndege la Ethiopia Ethiopian Airline , shirika kubwa la ndege barani Afrika  kwa upande wake limefahamisha kuwa linaendelea na safari zake kuelekea nchini China.

Imeripotiwa kuwa  abiria wote katika shirika hilo  wamechukuzwa afya zao.

Kulingana na vyazo kadhaa vya habari, idadi ya wasafiriki  kutoka China  kueekea barani Afrika  kwa sababu tofauti kama biashara au utalii  imekuwa abiria  1500 kwa siku.

China inajaribu kwa hali na mali kuzuia kile ambacho kinaonekana kuwa kama kizingiti katika ushirikiano wake na mataifa ya bara la Afrika katika sekta tofauti kutokana na virusi vya corona.

Viongozi ambao wanaakilishi China katika mataifa tofauti barani Afrika  wanaendesha mikutano ambayo  wanathibitisha kwamba  serikali ya china na wizara yake ya afya inawajibika ipasavyo  ili kuhakikisha virusi hivyo vinaangamizwa.

Mikutano na wanahabari,  hatua zilizochukuliwa na  China  zinatangazwa katika vyombo vya habari   barani Afrika.

Wanadiplomasia wa China wanazungumza kuhusu virusi vya corona katika  mataifa waliopewa wadhifa wa kuwakilisha  taifa lao.

Katika suala hilo, balozi wa China  nchini Afrika Kusini  amesema  kuwa waafrika wasiwe na hofu yeyote  kuhusu virusi hivyo.

Katika siku za hivi karibuni , virusi vya corona  vinapelekea China kuendelea kuangaliwa kwa jicho hasi .

China inajaribu kwa mbinu tofauti  kukabaliana na   jango hilo ikiwa pamoja na vyombo vya habari na njia ya diplomasia.

Mataifa ya bara la Afrika  yamefahamisha kuwa yapo bege kwa bege na China.

Kwa mfano, Guinea  imejitolea kiwango cha dola  milioni 2  kusaidia China katika juhudi za kupambana na virusi hivyo.

Licha ya  tahadhari kuchukuli  barani Afrika, tishio bado ni kubwa.

Sherika la afya la Umoja wa Mataifa  limefahamisha kuwa mataiga ambayo yapo katika hatari ni Algeria, Angalo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ethiopis, Ghana,   Côte d'Ivoire, Kenya,  Maurice,  Nigéria, Afrika Kusini  ,  Tanzanie,  Uganda   na Zambia Zambia.

Hofu hiyo ni kutokana na safari za hapa na pale kati ya China na mataifa hayo.

Katika mataifa ya bara la Afrika, vifaa vya matibabu vya kisasa  bado ni ndoto kwa mataifa mengi.
 Habari Zinazohusiana